Friday, March 12, 2010

MAPIGANO MAKALI YAENDELEA MJINI MOGADISHU

Milipuko, milio ya risasi na makombora imetanda katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu.
Makabiliano hayo yanaendelea kwa siku ya tatu mfululizo huku jeshi la serikali kwa ushirikiano na jeshi la kutunza amani la muungano wa Afrika, AMISOM, likiimarisha msako wake dhidi ya wapiganaji wa kiislamu.

Makombora, gruneti na silaha zingine nzito nzito zinatumika kwenye mapigano hayo. Soko moja maarufu mjini humo limeharibiwa kabisa.

Hakuna ripoti yoyote ya maafa iliyoripotiwa hii leo.Hapo jana watu 35 waliuawa kwenye mapigano hayo na wengine wengi kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment