Friday, March 12, 2010

HISTORIA FUPI YA MWANANDINGA DIDIER DROGBA



Akiwa amezaliwa Machi 11,1978 mjini Abidjan, jiji kuu la ivory Coast, Didier Drogba, alianza maisha yake ya dimba na klabu ya daraja ya pili ya Ufaransa, Le Mans.


Hakukawia kugonga vichwa vya habari katika msimu wa 2002-2003 alipopachika mabao 17 katika mechi 34 akiichezea klabu ya daraja ya kwanza ya Guingmp.


Mwaka huo, macho ya klabu maarufu ya ufaransa, Olympique Marseille,klabu ya muafrika mwengine Abedi Pele,yakamkodolea Drogba na akatia mabao 18 alipoisaidia timu hiyo kuingia finali ya kombe la ulaya la UEFA.

Mwaka uliofuatia , 2004 , salamu alizotoa Drogba huko Ufaransa, zikafika Premier League-Ligi ya Uingereza.Chelsea, ikamfungisha mkataba Drogba kwa kitita cha dala milioni 35.


Hakukawia pamoja na Chelsea kutwaa ubingwa wa Uingereza Premier League na kombe la League cup tena msimu wake wa kwanza tu huko Uingereza.Ni Drogba alielifumania lango la Liverpool katika finali ya Kombe la Ligi alipotia bao la ushindi baada ya kurefushwa mchezo na Chelsea kutamba kwa mabao 3:2, Drogba alikwsha kuwa maarufu hata Uingereza.

Msimu uliofuata ,Drogba akavaa taji jengine na Chelsea pale klabu hiyo ilipokuwa timu ya pili tu kuvaa taji la premier League kwa mwaka wapili mfululizo.

Kimataifa, Drogba alivaa jazi ya Ivory Coast, kwa mara ya kwanza Septemba 8,2002 pale Tembo walipocheza na Bafana bafana (Afrika Kusini).Drogba alitia bao lake la kwanza kwa timu ya taifa pale Tembo walipo wakanyaga simba wa nyika -Kameroun, hapo Februari 11, mwaka 2003 na kuondoka na ushindi wa mabao 3-0.

Halafu Drogba akapewa unahodha wa kuiongoza Ivory Coast katika Kombe la Mataifa ya Afrika hapo 2006,lakini jahazi lake lilienda mrama katika finali na mafarao Misri, mjini Cairo.

Baada ya kuachana sare 0:0 mikwaju ya penalty ilibidi kuamua hatima ya Kombe la Mataifa ya Afrika nahodha Drogba, akalizamisha jahazi lake pale mkwaju wake wa adhabu ulipokosea shabaha aliolenga.Furaha ilioje kwa mafarao na sultani wao wa dimba Hassan Shehata.

No comments:

Post a Comment