Saturday, March 13, 2010

KISS YAWATIA MATATANI

Raia wawili wa Uningereza wamejikuta wakipandishwa mahakamani kwa kosa la kupigana mabusu hadharani nchini Dubai.

Mkasa huo ulitokea katika mkahawa uitwao Packed Bob's Restaurant uliopo maeneo ya Jumeira beach, ambapo raia hao wa Uingereza walijikuta wakiwa mikononi mwa polisi baada ya mama mmoja ambae alikua na mtoto wake mdogo, alipowaona wakipigana mabusu kitendo ambacho kilimpelekea kupiga simu polisi na baadae polisi walifika kuwakamata.

Watu hao ambao wametajwa kwa majina ya Charlotte Lewis (25) pamoja na Ayman Najafi (24) walisema kitendo walichokifanya wao ni kua walipigana mabusu kwenye mashavu lakini mama huyo alisema yeye na mwanawe waliwaona wawili hao wakipigana mabusu kwenye midomo na kitendo hicho kilimtia mashaka mwanawe.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 38 alielezea mahakamani kwamba aliambiwa na mwanawe kwamba watu hao wanapigana mabusu kwenye midomo kabla ya yeye mwenyewe kugeuka na kuwaona kwa macho yake.

Pia mama huyo aliendelea kusema kwamba wawili hao walipeleka mikono yao chini ya fulana zao na baadae wakawa kila mmoja anampiga piga mwenziwe sehemu zake za nyuma.

Nae jaji Ebrahim Khalil Abuu Shamma alitupilia mbali dai la wawili hao kwamba Ayman alikua akimpiga busu Chalotte kwenye savu

Wawili hao wanaweza kuhukumiwa kwenda jela mwezi mmoja kila mmoja na baadae watarudishwa nchini kwao, kwa sasa wote wawili wamewekewa dhamana na hivyo wanaweza kukata rufaa mapema hapo kesho.

Chanzo kimoja cha sheria kinachohusika na kesi hio kimesema kwamba hakiamini kabisa kile ambacho kimewatokea wawili hao.


Ayman ambae ni mpenzi mkubwa wa timu ya Arsenal ya nchini Uingereza, kwa sasa anaishi Nchini Dubai ambapo alikwenda kwa ajili ya kufanya kazi katika shirika la Hay group, wakati Chalotte alikwenda kwa ajili ya holiday, ingawa haijuilikani kama Chalotte alikua akijuana na Ayman hapo kabla.

Siku za hivi karibuni kumekua na mfululizo wa kesi zinazo wahusu Waingereza Nchini Dubai.

Mwezi Januari mwaka huu iliripotiwa kwamba Mwanamke mmoja mwenye miaka 23 ambae pia ni Raia wa Uingereza aliwekwa kizuizini kwa kuambiwa kwamba alifanya mapenzi haram na mchumba wake, baada ya kuripoti kua alibakwa na mfanyakazi mmoja wa hoteli
waliyokua wamelala.

No comments:

Post a Comment