Thursday, March 11, 2010

MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALI ITB YAANZA BERLIN


Maonesho makubwa kaabisa duniani ya utalii yaitwayo ITB yanafunguliwa leo mjini Berlin hapa Ujerumani.Zaidi ya washiriki elfu 11 kutoka nchi zipatazo 180 wanashiriki katika maoensho hayo.

Wageni zaidi ya laki moja na elfu 70 wakiwemo watalaam wa sekta ya utalii wanatarajiwa kuyatembelea maonesho hayo yatakaydumu kwa muda wa siku tano.Katika maonesho hayo mwaka huu kutakuwa na nafasi maalum ya mjadala juu ya utalii, kuangalia uhusiano uliyopo kati ya utalii na mazingira.

Elimu ya uhusiano na viumbe na mazingira yaani Ikolojia, inataka utalii katika maeneo wazi ufanyike bila ya kuharibu uasilia wake.Barbara Engels ambaye ni mtaalam wa masuala ya utalii katika idara kuu ya hifadhi ya taifa mjini Bonn ana wasi wasi juu ya utalii usiyothamini mazingira.

´´Changamoto kubwa hii leo ni kwamba utalii ni sekta muhimu katika ukuaji wa uchumi.Hususan katika maeneo ya vijijini, ambako utalii huo wa katika maeneo ya wazi umekuwa ni chanzo muhimu cha mapato.Sambamba na kuongezeka kwa mahitaji ya utalii katika maeneo hayo, pia madhara ya uharibifu wa mali asili umeongezeka´´

Kila mwaka kwa mfano kiasi ya watu millioni 50, hutembelea mbuga za wanyama nchini Ujerumani.Pia katika maeneo mengine ya hifadhi idadi ya watu wanaotembelea imekuwa ikiongezeka.Dr Dominik Rossmann, ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya utafiti wa utalii na ushauri Ulysses Web Tourism, lakini pia ni mtalaamu katika idara hiyo kuu ya hifadhi za taifa ya Ujerumani.

Yeye anasema kuwa ni muhimu hata kwa wale wanaopata safari za mapumziko za bei nafuu katika maeneo ya Mediterrania kutilia maanani suala la mazingira.

´´Utalii na Mazingira ni vitu vilivyo na maingiliano,kwasababu utalii unasadia kuyalainda mazingira.Hakuna mtu anayependa kufanya mapumziko katika maeneo yaliyoathirika au yenye majanga.Watu wanataka kuiona dunia katika uasilia wake uliyo bora.Wanahitaji angalau kwa mwaka kupata wakati mzuri´´

Utalii ni maarufu sana, lakini pia kwa upande mwengine unachangia hatari ya kuharibu mazingira.Tayari usafiri unaotumika kuwafikisha watu katika maeneo ya vivutio vya utalii, umechangia kuharibu mazingira..Mjadala juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na umuhimu wa kupunguza utoaji wa gesi ya Carbon inayoharibu mazingira, umepelekea suala la mazingira kuwazindua wateja yaani watalii.Katika hili Dr Rossmann anasema.

´´Kuna kiwango kilichoweka cha gesi ya carbon itakayotoka kwa mtu mmoja kwa mwaka ambacho ni kiligram 3,000 kwa vipimo vya gesi.Kama utafanya safari ndefu, kwa mfano kuelekea Mexico au Amerika ya Kusini utakuwa tayari umetoa kwa mwaka mmoja pekee kiwango cha gesi ya Carbon ambacho ungekitoa kwa kipindi cha miaka miwili unusu´´

Mkuu wa maonesho ya ITB Martin Buck amesema kuwa mabanda yote 26 ndani ya uwanja huo wenye ukubwa wa mita za mraba laki moja na elfu 60, yamejaa.Amesema kwa mtu kutembelea maonesho hayo ya utalii ya Berlin basi atakuwa ametembea dunia nzima.

Nchi mshirika katika maonesho ya mwaka huu ni Uturuki, ambayo ni maarufu kwa watalii kutoka Ujerumani, Uingereza na nchi nyingine za Ulaya ya Magharibi.

No comments:

Post a Comment