Thursday, March 11, 2010

HATARI, UMEME MOTOT MOTO

Assalam aleykum.

Baada ya umeme kurejea katika kisiwa cha Unguja kwa masaa machache tayari Wazanzibari wengi wameingia katika majanga makubwa ya kupoteza vitu vyao vya umeme yakiwemo majiko ya umeme,pampu,runinga,majokofu na pasi.

Kwa sasa umeme huo umekuwa ukionekana kama hauna nguvu na wakati mwengine umekuwa ukiuona unaongezeka na kupungua na umekuwa ukizimwa mara kwa mara na majanga ya shoti ya umeme yamekuwa yakionekana katika mitaa mbali mbali huku kukiwa na habari kuwa baadhi ya maeneo yamepoteza waya za umeme kwa kuibiwa kutokana na baadhi ya vijana kuyayusha na kupata shaba iliomo ndani au kuziuza kwa watu wanazozihitajia wengi wa wakaazi wa manispaa ya mji wa Zanzibar wameanza kuchukua tahadhari.

Hata baada umeme kuwaka bado kuna maeneo bado umeme haujawaka kutokana na hitilafu za hapa na pale za kiufundi ni jambo zuri kuwasihi ndugu zetu kuacha kuviangamiza vitu vyao kwa kuacha kuwasha vitu vyenye thamani kubwa.

Mmoja kati ya viongozi wa ZEC amesema umeme huo ni mdogo ukilinganisha na ule tuliokuwa tukitumia kutokana na waya baada ya matengenezo hachukua kiwango cha zamani M 40 na utengezewa kiwango kilichobakia wa kutumia majenereta yatakapowasili.


Ahsante
Freedom Zenj.

No comments:

Post a Comment