Tuesday, March 2, 2010

HALA HALA UJITI NA MACHO!!!

RAIA NA VIONGOZI WA ZANZIBAR!

KUMBUKENI KUWA SINGAPORE ILIKUWA NCHI YA WAISLAM (WAMALAY). LEO HATA KUADHINI KWA SPIKA HAWATHUBUTU KWA KUPOTEZA HAKI ZAO KAMA RAIA. WACHINA (WAHAMIAJI) WAMEIFANYA SINGAPORE NI YAO NA WALE WAZALIA HAWANA HAKI TENA.

JEE NDUGU ZANGU VIONGOZI NA WAHUSIKA WA VITAMBULISHO, HAMUONI KUWA NA NYINYI MNAIPELEKA NCHI YETU YA ZANZIBAR HUKO TUNAKOKUOGOPA?

IKIWA HUAMINI HAYA, BASI NENDA PALESTINE! IKIWEMO HEBRON NA JERUSALEM. WAPALESTINA HIVI SASA SI MALI KITU. WAO NI WATU WA DARAJA LA TATU. WALA HAWAPEWI HAKI KAMA WANANCHI WA NCHI HIYO.

JEE MNATAKA NA SISI NA WATOTO WETU TUFIKISHWE HUKO?

WALLAHI, TENA WALLAHI, THUMMA WALLAHI, IKIWA MTAFANYA MCHEZO WA KUFIKIRIA MANUFAA YA NAFSI ZENU KABLA YA NCHI NA VIZAZI VYENU, BASI
NA SISI WAUNGUJA NA WAPEMBA HATUKO MBALI NA KUNYANYASWA NA WABARA KAMA WANVYOFANYIWA WAPALESTINA NA WAMALAY WA SINGAPORE KATIKA NCHI YAO WENYEWE.

KWA TAARIFA ZENU HATA KAZI, HATA UKIWA QUALIFIED VIPI, UKIWA SI MCHINA BASI HATA HAWAKUTIZAMI USONI, NA IKIWA SIO YAHUDI HATA HAWALITAZAMI HATA OMBI LAKO.

JEE MNATAKA KUFIKE HUKO? MKIENDELEA NA MTINDO KAMA HUU MNAOFANYA HIVI SASA , BASI NAKUAHIDINI TUMEKARIBIA NA TUTAFIKA HUKO SIO SIKU ZA MBALI HASA KWA VILE IMETOKEZEA HII RIZKI YA MAFUTA HAPA NYUMBANI. TAMAA YA MAFISI HAO ITAZIDI KUVIMBA.

JAMANI HALA HALA UJITI NA MACHO, NCHA UNA HO HO!!!!


INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO!

No comments:

Post a Comment