Friday, March 12, 2010

DROGBA ATANGAZWA MWANASOKA BORA BARANI AFRIKA

Mshambuliaji machachari kutoka katika timu ya Chelsea ya Uingeeza Didier Drogba ametangazwa kua ndie mwanasoka bora barani Afrika kwa mwaka 2009.

Drogba aliisaidia timu yake ya Ivory Coast kufuzu katika mashindano ya kombe la Dunia kwa kuifungia mabao matano katika mwaka wa 2009.

Tunzo hii ingekua ni muhimu kwa Mchezaji wa Inter Milan Samuel Eto'o ambae alitamani kuipata ili aweze kujiwekea rekodi ya kuitwaa kwa mara nne, ambapo aliwahi kuchukua katika mwaka 2003,2004,2005, ingawa yeye ndie mchezaji aliyewahi kuchukua tunzo hio kwa mara nyingi.

Lakini katika kura zilizopigwa na makocha ambao wanafundisha timu za Mataifa za Afrika zilimuwezesha Drogba kunyakua tunzo hio kwa mara ya pili baada ya ile ya kwanza kuchukua katika mwaka 2006, ambapo alishinda tunzo hio pale alipopata alama 76 na kumshinda Eto'o ambae alipata alama 74.

Eto'o ambae ametimiza miaka 29 wiki hii aliisaidia timu ya Barcelona katika fainali ya kombe la Champions League mweni may mwaka jana na kufanikiwa kuchukua kombe hilo, na pia alishinda tuzo ya heshima ya ligi ya Hispania kabla hajahamia Iternazionale Milan.

Eto'o pia aliipaisha timu yake ya Cameroon kileleni katika kufuzu kucheza Kombe la Dunia baada ya kocha mpya wa timu hio Paul le Guen kumchagua kua nahodha wa timu hio.

Kiungo machachari wa timu ya Chelsea nae alikua ni mtu wa tatu katika watu watatu bora ambapo alifanikiwa kuingia katika mzunguko huo wa tatu bora kwa mara ya tano, hajawahi kushinda tunzo hio hata mara moja.


Nae Mshambuliaji wa timu ya Manchester City Emmanuel Adebayor kutoka Togo ndie aliyejinyakulia Tunzo hio ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2008, wakati mshambuliaji wa timu ya Sevilla ya Hispania Frederic Kanoute alikua mwanasoka bora Afrika mwaka 2007.

Sherehe hizo za kumchagua mwanasoka bora narani Afrika zilifanyika nchini Ghana ambapo hakuna hata mshiriki mmoja aliehudhuria, ambapo timu ya Algeria ilitajwa kua ndio timu bora Barani Afrika
No comments:

Post a Comment