Friday, March 12, 2010

BABA NA MWANA KIZIMBANI KWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Baba mmoja na mwanawe wanatarajiwa kupandishwa mahakamani leo hii huko Tanga baada ya kukamatwa na kilo 95 za madawa ya kulevya aina ya heroine yenye thamani ya shilingi bilioni 25.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga alisema jana kwamba watu hawa wawili wa familia moja walikamtwa pamoja na watu wengine wanne akiwemo raia mmoja wa Iran huko Kabuku, Wilaya ya Handeni, siku ya Jumatatu.
Aliwataja watu hao waliokamatwa ikiwa ni pamoja na Bakari Kileo Mambo (75) mkaazi wa barabara ya 21 Tanga, Kileo Bakari (34) Mkaazi wa Mikocheni Dar-es-Salaam, Mohammed Ali (30) raia wa Iran, Yahaya Zume (30) Mkaazi wa Tanga, Salum Mohammed (35) mkaazi wa
Mbagala Dar-es-Salaam, na Said Ibrahim (33) mkaazi wa Bi Kinjuni Tanga.
Kwa mujibu wa taanrifa zilizopatikana, inasemekana kua Raia wa Iran aliingiza madawa haya nchini tarehe tarehe 31 machi mwaka huu kupitia Julius Nyerere Airport, na baadae kuunganisha na watuhumiwa wengine.
Jeshi la Polisi pia linashikilia gari mbili, Suzuki Grand Vitara yenye namba za usajili T 650 BAT pamoja na RAV4 yenye namba za usajili t 457 BCQ ambzo zilitumika kwa kuvushia madawa hayo.

No comments:

Post a Comment