Sunday, February 21, 2010

WAZIRI MKUU WA UHOLANZI BALKENENDE AWASILISHA BARUA YA KUJIUZULU

Waziri Mkuu wa Uholanzi, Jan Peter Balkenende amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia Beatrix wa nchi hiyo. Serikali ya muungano ya nchi hiyo imevunjika baada ya vyama viwili vikubwa kushindwa kukubaliana iwapo wawaongezee muda wanajeshi wake waliopo nchini Afghanistan.

Jumuiya ya Kujihami-NATO ilitoa ombi kwa Uholanzi la kuwaongezea muda wanajeshi wake walioko nchini Afghanistan hadi mwezi Agosti mwaka ujao.

Balkenende jana alitangaza kuwa serikali hiyo ya muungano iliyokaa madarakani kwa miaka mitatu imevunjika, baada ya mazungumzo ya muda wa saa 16 ya kuikoa serikali kumalizika bila ya mapatano yeyote. Kwa sasa Uholanzi ina wanajeshi 2,000 nchini Afghanistan chini ya vikosi vya kimataifa vya ISAF vinavyoongozwa na NATO.

No comments:

Post a Comment