Saturday, February 20, 2010

MNARA WA MSIKITI WAANGUKA NA KUUA WATU MOROCCO

Wafanyakazi wa huduma za uokoaji katika mji wa Meknes nchini Morocco wamekuwa wakiendelea na utafutaji wa manusura kufuatia kuanguka kwa mnara wakati wa swala ya Ijumaa.
Kwa uchache watu thelathini na sita waliuwawa na wengine zaidi ya sabini walijeruhiwa .

Inaarifiwa kuwa watu wengine zaidi wamefukiwa chini ya kifusi cha mnara huo.

Baadhi ya waokoaji wamekuwa wakijaribu kuwafikia manusura wakitumia mikono yao kwa sababu mashini kubwa na nzito haziwezi kupita kwenye barabara finyu za mji huo wa kale.

Maafisa walisema siku kadhaa za mvua kali ziliathiri mnara huo uliojengwa karne kadhaa zilizopita katika mji wa kihistoria wa Meknes.

No comments:

Post a Comment