Thursday, February 25, 2010

URAIA WA NCHI MBILI: TUKIZUBAA TUMELIWA !!

Binafsi sina tatizo kabisa na kuruhusu Watanzania kuweza kuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja (sielewi kwanini lazima uwe wa nchi mbili tu!) lakini kama unavyosema lazima tuweke wazi exceptions kwa sababu.. nakumbuka Fujimori kilipomuungulia kule Peru akakimbia nchi ya asili ya wazazi wake (Japani!) akidai uraia wa kule. Leo hii tunaona jinsi Wahaiti wenye uraia wa Marekani kilipoungua kule Haiti walivyokimbia kuonesha passport zao kuwa wao ni raia wa Marekani. Tumeliona hili hata kule Lebanon wakati mgongano kati ya Israel na Hezbollah. Tanzania itakuwa hivyo hivyo (tayari in some cases with some people in the Asian communities).

Tusipoweka mambo vizuri.. watawala wetu watakuwa ni raia wa nchi nyingine huku wakifanya mambo bila ya kujali maslahi ya nchi yetu hii kwani wanajua tukitaka kuwatia pingu wanaonesha passport zao au zile za watoto wao na kutimka kwenda "kwao"!

so.. tunaporuhusu uwezekano wa mtu kuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja ni lazima wakati huo huo tuainishe vizuri kabisa mipaka ya jambo hilo. Sasa kama wakati huu ambapo hatuna sheria hiyo na tunajua kuwa mtu akiwa na uraia wa nchi nyingine anakuwa ameuakana uraia wetu inakuwaje katika akili timamu tunampendekeza kutuwakilisha kwenye nchi nyingine wakati siyo raia wetu!?

Kuna watu ambao walikuwa karibu sana na serikali yetu kwa miaka mingi baada ya mambo kutulia kwenye nchi zao wakafunga virago na kurudi "kwao" a.k.a Wanyarwanda tuliowadhania ni Waangaza!

Mimi sipingi uraia wa nchi mbili at all.. napinga kanuni zinazopendekezwa. Hatuwezi kubadilisha nature ya uraia wetu kwa sababu ya rangi, nasaba, hali ya kiuchumi, kufuata mtindo n.k.. we have to articulate proper arguments why we have to change.. siyo nchi zote duniani zinaruhusu uraia wa nchi mbili hata zile za kiafrika au za kimagharibi. Sielewi kwanini tuonekane tunafuata zile za nchi fulani na zile za nchi nyingine tuone hazifai.

Chanzo: Mwanakijiji

No comments:

Post a Comment