Thursday, February 25, 2010

SARKOZY KUWASILI RWANDA

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa anawasili leo nchini Rwanda katika ziara yenye nia ya kurejesha uhusiano mwema kati mataifa hayo mawili, ambao uliharibika kutokana na mauaji ya halaiki nchini humo ya mwaka 1994.


Sarkozy anakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kuizuru Rwanda tokea mauaji hayo, ambapo zaidi ya watutsi laki nane na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa katika kipindi cha siku mia moja cha mauaji hayo.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ulivunjika mwaka 2006, baada ya jaji mmoja wa mahakama ya Ufaransa, kumtuhumu Rais Kagame kuwa alipokuwa kiongozi wa waasi alichangia mauaji hayo kwa kushiriki kwake katika kutunguliwa kwa ndege aliyekuwemo Rais wa wakati huo Juvenal Habyarimana.

Rais Sarkozy anawasili Rwanda akitokea Mali alikofanya ziara ya kushtukiza, na kukutana na mateka wa kifaransa Pierre Camatte aliyeachiwa huru na wapiganaji wa tawi la al Qaida la Afrika Kaskazini.Kabla ya hapo aliizuru Gabon

No comments:

Post a Comment