Friday, February 12, 2010

UINGEREZA NA RWANDA KUBADILISHANA WAFUNGWA

Makubaliano ya kukabidhiana wafungwa kati ya Rwanda na Uingereza yametiwa saini na waziri wa sheria wa Rwanda, Tharcis Karugarama na Balozi wa Uingereza nchini Rwanda, Nicolus Cannon Rwanda .
Makubaliano hayo yataruhusu watu waliohukumiwa na mahakama katika yoyote ya nchi hizo kutumikia kifungo nyumbani.

Rwanda ndiyo nchi ya pili ya kiafrika kutia saini makubaliano hayo na Uingereza, baada ya Uganda kusaini makubaliano kama hayo mwaka jana.

Wachambuzi wanasema Rwanda inataka kuonyesha jamii ya kimataifa kwamba inaweza kupokea watu waliohukumiwa na mahakama ya kimataifa ya Rwanda ambayo inasikiliza kesi za washukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 94.

Mahakama hiyo iliyo mjini Arusha, Tanzania, imekuwa ikikataa kuwakabidhi watu iliowahukumu kwa serikali ya Rwanda, ikidai kuwa mfumo wa gereza wa taifa hilo, hauwahakikishii haki wafungwa hao.

No comments:

Post a Comment