Friday, February 12, 2010

SALAAM ZA IJUMAA - SHAIRI

JUMA'A KAREEM!!

Wapendwa iwe ni ada Istawi Ukumbini
Iwe yetu kawaida Siku hii tupambeni
Au pawekwe kasida Waungwana nambieni
Kina kaka kina dada Fursa itumieni

Kuingia Ijumaa Furaha ziwe moyoni
Haitofaa hadaa Allah tumuogopeni
Sura zisije kunyaa Ukatiwa kaburini
Hakuna lakukufaa Utakuwa hasarani

Mikono juu kwa dua Jalali tumuelekeni
Tupate nyingi shufaa Ibada tuongezeni
Hakuna cha kuzubaa Hili tueke usoni
Machozi husaidia Pindi upo duniani

Watu wakikufukia Chozi litafaa nini
Ni bora kukuzindua Kuliko kukuacheni
Babengwa namalizia Itikieni amini
Tuombeni nyingi dua Ili tulale peponi.

Waislamu sote ukumbini, tutakieni kila la kheri

Maasalaam,

Babengwa Zanzibar

No comments:

Post a Comment