Assalam aleykum
Enzi tulipokuwa wadogo, ilikuwa wali unapambiwa kwa mkungu, unafanya gamba (matandu) ya brown, mpunga mpya unanukia
Vile vile vijana walikuwa wanakung'utia maji ili yaonekane makaa yashamaliza kazi
Wapi, utamaduni umepotea! watu wote wanapiga rice cooker, wali si wali, bonndo si bondo, ni balaa tu.
Mchuzi pia ukipikwa kwa vyungu waweza ukajiramba, lakini wapi, watu wote tumejaa maluminium miili mwetu
Jee tunakwenda mbele au twarudi nyuma? Iko haja ya kudumisha mila.
***Mpitanjia
No comments:
Post a Comment