Friday, February 26, 2010

BARUA YA PAPII KOCHA KWENDA KWA JK

MF/NA: 836’04 Johnson Nguza (Papii Kocha)

Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam

Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika Gereza Kuu Ukonga.
Kwa heshima na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliyokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naanguka na kushika miguu yako mitukufu mheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.

Mh. Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatma pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.
Naomba huruma yako mheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninayehitaji huruma yako wewe mzazi.

Natumaini kauli yako ya mwisho ndiyo itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki

Wako mtiifu
NO:836’04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

No comments:

Post a Comment