Saturday, February 20, 2010

TIGER WOODS AMUANGUKIA MKEWE

Mcheza gofu mashuhuri duniani Tiger Woods katika mkutano wa waandishi wa habari amemuomba radhi rasmi mkewe kwa kumuendea kinyume.

Mcheza gofu huyo anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa ubora duniani, alikuwa akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kashfa iliyokuwa imegubika maisha yake ya faragha kuibuka mwezi wa Novemba mwaka jana.

Woods Mmarekani mwenye umri wa miaka 34 alikuwa akihutubia kundi dogo la marafiki, wacheza gofu wenzake na jamaa wa karibu mjini Florida.

Mcheza gofu huyo aliyewahi kushinda mataji makubwa mara 14 alisema hakuwa mwaminifu, alikuwa na uhusiano na wanawake wengine na alitembea nje ya ndoa. Alikiri kitendo hicho ni cha fedheha na hakikubaliki.

Aliendelea kukiri, kwa vitendo vyake amemuumiza mkewe, wanawe, mama yake, familia ya mkewe, mfuko wake na watoto wote duniani waliokuwa wakimpenda.

Woods alisema kuna uwezekano wa kurejea kucheza tena gofu mwaka huu, lakini akasema bado hajapanga tarehe na akaongeza atarejea tena kupata nasaha na ushari siku ya Jumamosi.

Alisema ni vigumu kukiri lakini anahitaji msaada.

Tiger Woods alifafanua kwamba kwa siku 45 tangu mwishoni mwa mwezi wa Desemba hadi mapema mwa mwezi wa Februari, alikuwa akipatia matibabu ya kitaalamu ya kumuweka sawa na dhoruba hiyo ya maisha aliyokumbana nayo.

Alisema anasafari ndefu katika hilo lakini amekamilisha hatua ya awali ya safari hiyo kwa njia sahihi.

No comments:

Post a Comment