Saturday, February 20, 2010

SERIKALI YA MUUNANO YA UHOLANZI YAVUNJIKA

Serikali ya muungano ya Uholanzi imevunjika baada ya vyama viwili vikubwa kushindwa kukubaliana endapo wawaondoe wanajeshi wake nchini Afghanistan au la mwaka huu kama ilivyopangwa.

Baada ya mazungumzo yaliyofanyika majira ya usiku mjini The Hague pamoja na baraza la mawaziri, Waziri Mkuu wa Uholanzi Jan Peter Balkenende ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo imeshindwa.

Baraza la mawaziri limekuwa likijadili ombi lililotolewa na Jumuiya ya Kujihami-NATO kwa Uholanzi kuwaongezea muda wanajeshi wake walioko nchini Afghanistan hadi mwezi Agosti mwaka ujao wa 2011.

Chini ya serikali ya sasa, wanajeshi 2,000 wa Uholanzi walioko katika vikosi vya NATO vinavyoongozwa na ISAF nchini Afghanistan wanatakiwa kuondoka katika jimbo la Uruzgan mwaka huu.

No comments:

Post a Comment