Friday, February 19, 2010

CONGO YAFUNGA MAKANISA NA VILABU VYA POMBE MJINI KINSHASHA

Makanisa manane pamoja na vilabu vya kuuza pombe kadhaa vimefungwa mjini Kinshasa (DRC) kwa kuhusika na kelele za usiku na mchana.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na serikali imelalamikiwa na wafuasi wengi wa makanisa hayo ambao wamehisi kwamba viongozi walitakiwa kupiga marufuku kelele na sio kufunga makanisa.

Kumejitokeza jijini Kinshasa miaka ya hivi karibuni mfumuko wa makanisa ya kujitegemea ambayo yanajiita makanisa ya muamko ama " wake up churches." Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo.

No comments:

Post a Comment