Saturday, February 13, 2010

HARUSI YA WANAUME YAVUNJWA MOMBASA

Polisi katika mtaa wa Mtwapa ulioko kaskazini mwa mji wa Mombasa nchini Kenya wamewakamata wanaume wawili waliokuwa wanajiandaa kuoana.

Afisa wa utawala katika eneo hilo George Matundura amesema wanaume hao walikuwa na pete tayari kufunga ndoa katika hoteli moja iliyoko Kikambala katika wilaya jirani ya Kilifi.

Raia pia wameripotiwa kuwakamata wanaume wengine kadha wanaodaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja na kuwakabidhi kwa Polisi.

Ndoa za watu wa jinsia bora ni marufuku nchini Kenya, lakini sio jambo la kawaida wale wanaofanya hivyo kukamatwa.

Makundi ya Waislamu na Wakristo katika eneo hilo walifanya maandamano wakilaani kile walichokielezea kuwa tabia ya baadhi ya watu isiyokubalika katika eneo hilo la Mtwapa.

No comments:

Post a Comment