Thursday, February 4, 2010

RAIS OBAMA ALAANI MUSWADA WA UGANDA

Rais wa Marekani Barack Obama amekosoa pendekezo la sheria lililotolewa Uganda la kupinga mapenzi ya jinsia moja na kulieleza kuwa jambo la kuchukiza.
Muswada huo unapendekeza mwenye hatia kufungwa jela kwa muda mrefu au hata adhabu ya kifo katika baadhi ya matendo hayo ya jinsia moja.

Bw Obama amewaambia wanasiasa na viongozi wa dini katika maombi ya kitaifa ya Marekani mjini Washington, "Kuwalenga wapenzi wa jinsia moja kwa jinsi walivyo ni kuvuka mipaka".

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja tayari ni kinyume na sheria nchini Uganda na adhabu yake ni kifungo jela kwa takriban miaka 14.

Mswada huo unatarajiwa kuongeza uzito wa adhabu hiyo kwa kupewa kifungo cha maisha.

No comments:

Post a Comment