Friday, February 5, 2010

SARATANI YA KIZAZI YAKITHIRI TANZANIA

Tanzania imekuwa ikipoteza watu 30,000 kati ya 40,000 kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani.
Wanawake ndio wanaotajwa kuathirika zaidi kwa saratani ya shingo ya kizazi.

Kutokana na Tanzania kuwa na hospitali moja tu ya kutibu maradhi hayo iliyopo mjini Dar Es Salaam wagonjwa hulazimika kulala chini kutokana na msongamano.

Wengine hutibiwa majumbani kwa ukosefu wa nafasi za kuwalaza.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya saratani Tanzania, Dr Twalib Ngoma amesema wazazi washauriwe kuwapa chanjo watoto licha ya kuwa gharama kubwa.

Gharama ya chanjo hiyo ni dola 900 sawa na zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili za kitanzania.

No comments:

Post a Comment