Wednesday, February 17, 2010

NEC INA AJENDA MBAYA KWA ZANZIBAR - MZANZIBARI ZINDUKA

Kila kunapo kucha hali ya Zanzibar inabadilika kutokana na joto la uchaguzi hapo mwezi oct. Vile vile kuna wengine wana furaha kutokana na maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa visiwani humo kwamba yanaashiria njozi njema.

Lakini kuna upande mwengine, hali imeshaaza kuwa ya wasi wasi wakifikiria yale masahibu yanayowakuta kila baada ya miaka mitano.

Mara nyingi kwa nchi zenye demokrasia ya kweli,wananchi wake huwa wanapendelea kipindi kama hichi. Utaona wanaopigania uongozi wakielezea mipango yao au sera zao kwa wananchi juu ya maendeleo na huduma nyengine za kijamii. Kwa upande wa Zanzibar hali sio shuari kwani huu ni wakati wa majonzi na adhabu kubwa kwa wanajamii.

Hatuna budi kuwapongeza wale wote ambao wanachukua juhudi za mak-sudi kutaka kuviepusha visiwa hivi na balaa inayoandaliwaa huko mbele na Tume ya uchaguzi (ZEC).

Ni ukweli usioweza kupingika kwa mtu yeyote, kwamba upepo wa mabadiliko umevuma Zanzibar, na tayari watu wanajiandaa kuona Zanzibar mpya, kwani wako hoi bin Taaban kimaisha na vurugu zisizo msingi za kila siku kwa maslahi ya makaburu wachache wasiotakia mema visiwa hivi.

Ingawaje kama nilivyoeleza katika nakala zilizopita kwamba wako wachache wasio ridhishwa na hali ya matokeo mazuri ya maridhiano yalio jitokeza kati Maalim SEIF na MH. Abeid Aman. Watu hawa wanahaha kuona hali inatibuka na wao wanaendelea kuzifurahisha nyoyo zao na ndoto zisizokuwa na kikomo za madaraka na ving’ora.

Ili uchaguzi uwe huru na haki basi hauna budi kusimamiwa na chombo maalum na sio ZEC. Kwani tume inayoongozwa na Usalama wa Taifa, ndio chanzo cha fujo katika chaguzi zote zilizofanyika huko nyuma. Sasa iweje leo hii, wasimamie kura za maoni na uchaguzi wa visiwa hivi na wao ndio chanzo cha matatizo?

Nawatahadharisha wale viranja wote wanaoshabikia uonevu na uporwaji wa haki ya wazanzibar, kwamba kila kitu kina mwanzo na mwisho wake na mara hii wasitegemee kwamba itakuwa rahisi kama hivyo walivyozoea. Najua mazoea yana tabu lakini mpaka tabia ziwe zinalingana. Na tayari mwendo wa tume hauridhishi kabisa , kwani hawafanyi kazi kama tume huru na bali wanaongozwa na idara ya usalama wa Taifa sasa niambieni hapo jamani haki itatendeka ?

Tunakuomba Rais Kikwete hili uliangalie kwa mapana kwani bila kulifanyikia kazi historia katika uongozi wako itakumbwa na doa jeusi kama alivyofanya Benjamin Mkapa katika uongozi wake.

Licha ya ubadhirifu wa fedha na kashifa ya rushwa katika uongozi wake pia damu ya wazanzibar ilimdondokea yeye akiwa Amir Jeshi Mkuu kwa amri yake. Kikwete tunajua wewe ni muungwana hatutegemei kwamba utatufikisha huko.

Tulio wengi Zanzibar hatuna imani na tume hii. Ni ajabu na vichekesho kuona kwamba hapo zamani Wazanzibar wakiibiwa kwa kura na kubadilishwa matokeo, kama hivyo haitoshi mara hii hata kuundikishwa basi wanakoseshwa haki yao sasa hii tume tuielewe vipi?

Huyu anaenyimwa hakli ni mzanzibar halisi, nawauliza ZEC muna agenda gani kwaWazanzibar? Musijenge zana kuwa hali itakuwa shuari kama mutakataa matakwa yawalio wengi, jitayarisheni kwa kuwamaliza Wazanzibar kwa mtutu wa bunduki kama mulivyofanya huko nyuma.

Mungu libariki Taifa la zanzibar -Amini

No comments:

Post a Comment