Wednesday, February 17, 2010

ASKARI KANZU NA WENGINE WANNE KUTUPWA JELA MIAKA 25

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Ruvuma, imewahukumu kifungo cha miaka 25 jela watu watano akiwemo aliyekuwa akari kanzu a jeshi la polisi Kituo cha Mbamba Bay, Koplo Dustan Mweta (25) kwa kosa la kuvunja na kuiba briefcase iliyokuwa na camera yenye thamani ya dola 1,350 za Marekani Euro 800, simu za mikononi tano na Sh. 1,510,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh. 5,040,000 mali ya Emanuel Masanche mmiliki wa Nyasa View Hotel Mbamba Bay.

Waliohukumiwa kifungo hicho ambapo kila mmoja atatumikia miaka mitano ni mhudumu wa Hoteli ya Nyasa View, Susana Kapinga (25), John Yona (30), mkazi wa Mbamba Bay, Gallus Mchimbi (36), mkazi wa Mbinga mjini, Joseph Mbunda na Koplo Mweta.Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi a Mahakama ya Mkoa, Baptist Mhelela, alisema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na mashahidi wanne.

Hakimu Mhelela alisema kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitano jela kutokana na ushahidi ambao umeonyesha kuwa ulikuwa na mazingira ya wizi uliotokea kwenye Hoteli hiyo.

Alisema wahtakiwa wamepewa adhabu hiyo ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia mbaya kama hiyo na haa ikizingatiwa kuwa askari polisi imeonekana alihusika kupanga njama za kuvunja na kuiba.

Awali, ilidaiwa na mwanasheria wa Serikali kuwa Desemba 25, mwaka juzi, katika mji mdogo wa Mbamba Bay kwenye Hoteli ya Kitalii ya Nyaa View ambayo ipo kando kando ya ziwa Nyasa, washtakiwa wote watano walipanga njama na kuvunja na kuiba briefcase ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye moja ya vyumba vya Hoteli hiyo na kuiba vitu na fedha hizo.

Hata hivyo, washtakiwa kwa mara ya kwanza walikana mashitaka hayo na kwamba kesi iliendelea kusikilizwa hadi ilipofikia hukumu hiyo.

No comments:

Post a Comment