Wednesday, February 24, 2010

MIGOMO YA NDEGE BARANI ULAYA

Waongozaji safari za ndege nchini Ufaransa wameanza mgomo wao wa siku nne, kupinga wazo la kuunganisha mamlaka za kimataifa zinazosimamia safari za ndege. Ubelgiji, Ufaransa,

Ujerumani, Luxembourg, Uholanzi na Uswisi wana mpango wa kuunganisha mamlaka zao za safari za ndege ili kuimarisha usalama na pia kupunguza gharama.

Hata hivyo kuna uwezekano wa kufanyika mgomo wa wahudumu wa Shirika la ndege la Uingereza British Airways, hapo kesho wakitaka nyongeza ya mishahara.

Kiasi cha wafanyakazi milioni tatu nchini Ugiriki wanatarajiwa kushiriki katika mgomo wa kitaifa hii leo. Vyama vya wafanyakazi vinataka mapendekezo ya hatua kali za kurekebisha uchumi kutupiliwa mbali. Mapendekezo hayo ni pamoja na hatua ya kusimamisha nyongeza za mishahara pamoja na kuongezwa kwa kodi.

Mgomo huo wa sekta za umma utasababisha kufungwa kwa shule, hospitali na afisi za serikali pamoja na kutatiza shughuli za usafiri. Mgomo huo unakuja wakati Maafisa wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Athens kuangalia vipi watapunguza upungufu mkubwa uliopo katika bajeti ya serikali ya Ugiriki.

No comments:

Post a Comment