Saturday, February 27, 2010

MECHI ZA LEO

Mechi inayotarajiwa kua nzuri na ya kuvutia ni kati ya Chelsea watakapo wakaribisha Man City katika uwanja wao wa nyumbani huku mechi hio ikiwa na wasi wasi kwa timu zote mbili kwani timu zote mbili zitawakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu.

Chelsea watamkosa mlinda mlango wao nambri moja petr Cech ambae anasumbuliwa na misuli ambapo wantarajiwa kumchezesha mlinda mlango wao nambari mbili Hilario.

Mlinzi wa kushoto wa Chelsea na timu ya taifa Uingereza Ashley Cole ambae pia ni mgonjwa wa ancle kwa muda mrefu nae nafasi yake itachezwa na Malouda, lakini kama hii haitoshi Chelsea pia wana tatizo la viungo wao wawili Deco, Essien pamoja na mlinzi wao wa kulia Bosingwa ambao wote wanasumbuliwa na magoti.

Lakini pia kwa upande wa wageni City nako hali sio nzuri kwani wanataria kuwakosa wachezaji wao kadhaa muhimu kama vile mshambuliaji machachari Emmanuel Adebayor ambae anatumikia adhabu ya kutocheza mechi tatu.

Mlinzi Kolo Toure anaendelea kukaa juu kutokana na tatizo la goti, Santa Cruz nae pia atakosa mechi ya leo kwa kua na tatizo hilo hilo la goti huku kiungo Patric Vieira nae akikosa mechi ya leo kutokana na kutumikia adhabu yake ya kutocheza mechi tatu.

Lakini Man City wataweza kufaidika katika mechi ya leo kwani wataweza kumchezesha mshambuliaji wao Carlos Tevez ambae amesharejea kutoka Argentina ambako alikwenda kwa sababu ya mambo ya kifamilia.


Premier League
13:45 Chelsea v Manchester City
16:00 Birmingham City v Wigan Athletic
16:00 Bolton Wanderers v Wolverhampton Wanderers
16:00 Burnley v Portsmouth
16:30 Stoke City v Arsenal

La Liga
18:00 Getafe CF v Real Zaragoza
20:00 CD Tenerife v Real Madrid
22:00 FC Barcelona v Málaga CF

Bundesliga
15:30 VfL Bochumvs1. FC Nürnberg
15:30 Hertha BSCvsHoffenheim
15:30 FSV Mainz 05vsWerder Bremen
15:30 VfB StuttgartvsEintracht Frankfurt
15:30 Borussia MönchengladbachvsSC Freiburg
18:30 Bayer Leverkusenvs1. FC Köln

No comments:

Post a Comment