Saturday, February 27, 2010

CHEKA KIDOGO - KILIMO CHA MTAKULA ZANZIBAR

Wakati wa aboud Jumbe, alitoa maagizo kwa wananchi kuwa kuna mradi wa MTAKULA, maana yake ni kuwa kila familia au nyumba lazima wawe na shamba la migomba 300.

Katika kijiji kimoja pale Pemba (Mtambile kuna jamaa mmoja alikuwa hashughuliki na suala hilo la kupanda migomba.

Akiamka anakwenda katika charahani yake anashona na jua likitua anarejea kwake.

Sheha wa pale alikuwa ni mtu mkorofi na alikuwa haipendi ngozi nyeupe, basi akamtomeza mkuu wa wilaya kuwa kuna mtu hataki kulima na kufuata maagizo ya Mtakula. Ukapangwa mkakati wa mkuu wa wilaya kuja kufanya ukaguzi wa migomba mtambile, lakini lengo lilikuwa nikutaka kutia hatiani jamaa huyo.

Bhati katika baraza la pale kijijini, mmoja wa wajumbe wake (balozi) ni ngozi nyeupe na yeye, na akamjulisha jamaa kuwa unakuja kukaguliwa fanya bidii upate migomba 300.

Fundi charahani huyo hakuwa na wasi wasi na alimjibu balozi kuwa hamuna wasi wasi wacheni muje tu, Balozi alishangaa kusikia hivyo kwa vile fundi huyu anajulikana hajashikapo jembe zaidi ya charahani yake.

Mkuu wa wilaya Ali Mussa akaja Mtambile na kaanza kufanya ukaguzi kwa baadhi ya watu kisha wakamwendea fundi.

Huyu fundi alikuwa akikaa karibu na kitua cha polisi, lakini akishona karibu na kiunga cha famili Mtambile mjini na ni nyuma tu ya hapo anaposhona.

Sheha: Fundi mhe. mkuu wa wilaya anataka kuona migomba yako 300

Fundi: sawa twendeni hapo nyuma.

Walipofika:

Fundi: Ingieni humu katika shina la kijakazi hesabuni mia 300 kama haijatosha nitawapeleka sehemu nyengine pale chini.

Mkuu wa Wilaya: Umetakiwa ulime migomba 300 ya ndizi mbali mbali siyo aina moja.

Fundi: Maagizo yaliyotolewa yamesema migomba 300 tu na siyo migomba maalum.

Balozi pale alipo anataka kupasuka mbavu kwa kuchekea ndani kwa ndani, na yule mkuu wa wilaya alihamaki akapanda gari akarudi Mkoani.

Shina moja la migomba hiyo ilikuwa ni zaidi ya elfu wakati huo na alikuwa nayo matatu pale.

No comments:

Post a Comment