Friday, February 19, 2010

JESHI LATWAA MADARAKA NIGER

Jeshi nchini Niger limethibitisha kuwa limetwaa madaraka na limetangaza kuivunja serikali ya nchi hiyo. Pia Rais Mamadou Tandja pamoja na baraza lake la mawaziri wanashikiliwa.

Msemaji wa wanajeshi waliotwaa madaraka, Kanali Goukoye Abdul Karimou, alijitokeza katika televisheni ya nchi hiyo kutangaza mapinduzi hayo.

Kufuatia mapinduzi hayo ya kijeshi huko Niger, Umoja wa Afrika umelaani hatua hiyo, ambapo Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Jea Ping, amesema kuwa wanaifuatilia kwa karibu hali nchini humo.

Mapinduzi hayo yamefanyika huku kukiwa na hali tete ya kisiasa, baada ya Rais Mamadou Tandja kuongezewa muda wa kukaa madarakani .

August mwaka jana, Rais Tadja alilivunja bunge pamoja na mahakama ya katiba, ili kushinikiza mabadiliko ya katiba yatakayomruhusu kuweza kuwania tena urais hata baada ya kumaliza vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Na taarifa za hivi punde zinasema kuwa wanajeshi waliyotwaa madaraka wamemtangaza kiongozi wao kuwa ni Salou Djibo.

No comments:

Post a Comment