Friday, February 5, 2010

KARATA TATU DARAJANI USIKU

Assalaam alaikum
Hakuna mchezo mbaya kati ya michezo ya hadaa ambao ni wizi mtupu kama karata tatu, mchezo huu huchezwa kwa kutumia vibiriti ama kifunikio vya chupa, ambapo kundi la vijana kama 7 hukaa pamoja ili kuvutia watu.
Huku wajifanya nao ni wateja huku wakijishindia pesa na unapokaribia wewe huvutika na kuanza kuchagua kibiriti chenye njiti kwa kubadilishwa cha kati kuletwa kushoto na cha kushoto kati au kulia.
Baada ya kwisha hutulia na kukutaka uchague chenye njiti hapo huchagua chenye njiti na kukuonyesha umeshinda toa elfu 10000 ushinde elfu 40000, na ukiwa mbioni kujifundua mmoja wao hukupiga kibega na unapoangalia basi haraka hubadilishwa na baada ya kutoa pesa basi huwambiwa umekosa jaribu bahati yako tena.
Na unapotaka kuleta fujo basi hudhibitiwa na hata kupigwa mateke huo ni mmoja kati ya michezo ya wizi ya Kitanganyika au wabongo na sasa mchezo huu huchezwa Darajani usiku karibu na duka la madawa la Fahud.

Wazanzibari amkeni!!!

No comments:

Post a Comment