Friday, February 5, 2010

WAMAREKANI WAKUTWA NA MAKOSA YA KUTEKA WATOTO HAITI

Wamisionari 10 wa Kimarekani wameshtakiwa kwa makosa ya kujaribu kuwateka nyara watoto 33 wa Haiti, wakitumia mwanya wa tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Haiti mwezi uliyopita.

Wamarekani hao wanaume watano na wanawake watano, walizuiwa na kukamatwa katika mpaka wa nchi hiyo na Jamuhuri ya Dominica wakati walipokuwa wakijaribu kuvuka mpaka huo wakiwa katika basi pamoja na watoto hao.

Watuhumiwa hao ambao wengi wao ni watumishi wa kanisa katika jimbo la Idaho nchini Marekani, wamesema kuwa walikuwa wakijaribu kuwaokoa watoto hao waliyotelekezwa na ambao walikuwa ni mayatima, na kwamba hawakujua kuwa walikuwa wakitenda kosa la kihalifu.

Iwapo watapatikana na hatia wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 15 gerezani.Tetemeko hilo nchini Haiti limesababisha takriban watu millioni moja kukosa makaazai na wamekuwa wakiishi mitaani.

No comments:

Post a Comment