Wednesday, February 17, 2010

ZIMBABWE HAITISHWI NA VIKWAZO ZAIDI

Chama tawala cha rais Robert Mugabe wa Zimbabwe; ZANU-PF, kimepuuzilia mbali kurefushwa muda wa vikwazo vilivowekwa na nchi za Umoja wa Ulaya, kikidai ni njama ya ushirikiano na chama tanzu kliomo katika serikali ya muungano ya nchi hiyo.

Msemaji wa ZANU-PF, Rugare Gumbo, amesema hawana wasiwasi na kurefushwa muda wa vikwazo hivyo, na kwamba wataendelea na jitihada zao za ukombozi. Alisema ni dhahiri shahiri watajikomboa wenyewe.

Bwana Gumbo alikilaumu chama cha Movement for Democratic Change, MDC, kinchoongozwa na waziri mkuu, Morgan Tsvangirai, kwa kuunga mkono vikwazo hivyo dhidi ya rais Mugabe na marafiki wake wengine wa kisiasa mia moja.

Mwezi Septemba mwaka jana, Umoja wa Ulaya ulituma wajumbe wake nchini Zimbabwe na katika tathmini yao hawakuridhishwa na mwelekeo wa mabadiliko. Shirika la kutetea haki za kibinaadam la Human rights Watch lilipendekeza kuongezwa muda wa vikwazo kutokana na visa vya kukiukwa haki za binadamu, vikiwemo mauaji ya wakereketwa wa chama cha upinzani.

No comments:

Post a Comment