Saturday, January 2, 2010

MWANAMKE AJIFUNGUA WATOTO WAKIWA WAMEUNGANA ZANZIBAR

Mwanamke mmoja mjini Zanzibar Farihati Maulid (18) amejifungua watoto mapacha walioungana Usiku wa Mwaka mpya.

Mwanamke huyo alijifungua kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Mnazi Mmoja leo saa tatu Asubuhi na mapacha hao wako katika chumba cha uangalizi maalum wakisaidiwa kupumua kwa mashine. Mkunga wa Hospitali hiyo, Halima Habib Abdallah, na Dk. Mwana Omar, mkuu wa Kitengo cha uzazi wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema tukio hilo ni la kwanza na wanaendelea kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wengine wa Afya.

Mapacha wote ambao ni wa kiume wenye moyo mmoja, wameunganika kuanzia kwenye kitovu hadi kwenye mfupa wa Kidari wana uzito wa kilo 2.8 na kutokana na kutumia moyo mmoja inaonekana itakuwa vigumu kuwatenganisha.

Habari zaidi zinasema mama wa watoto hao ni mkazi wa Mwanyanya, Bububu katika Manispaa ya Zanzibar na uzazi huo ulikuwa wa kwanza.

No comments:

Post a Comment