Saturday, January 2, 2010

UGOMVI WA NDUGU

Hivi karibuni tulishuhudia mkasa wa mzungu mmoja "mjeuri na fedhuli" ambae alikumbana na kijana wa kiunguja ambae alimuweka sawa jeuri zote zikamwishia.


Mkasa wenyewe ulianzia hivi:

Mzungu alikua na Kima (Tumbili) wake akitembea nae. Hapo palikua na kijana anauza matunda, zikiwemo ndizi. Yule mzungu hakumdhibiti yule kima wake na kima akarukia zile ndizi akachukua moja akala. Kijana akaomba alipwe na mzungu akalipa.

Lakini mchezo haukuishia hapo, ikawa kila mara yule kima hurukia na kuchukua ndizi nyengine, mara ya pili, ya tatu.... mwisho mzungu kwa jeuri yake tu akakataa kulipa tena, na alipoulizwa kwa nini hataki kulipa akajibu "KWANI SI KACHUKUA CHA NDUGU YAKE TU" (akimaanisha yule kijana na huyo kima ni jamii moja).


Yule kijana kusikia kwamba kajibiwa kauli hiyo kwanza alishangaa, lakini hakugombana. Alivuta akili na baada ya muda yule kima akaparamia tena meza ya yule kijana ili kuchukua ndizi nyengine. Kijana hakufanya ajizi... alimpiga kima kipanga kimoja tu, akamjeruhi vibaya sana.


Mzungu kuona hivyo alibadilika rangi akawa mweusi kwa hasira, na alipolalamika kijana akasema mwambieni mzungu - "UGOMVI WA NDUGU ASIUINGILIE"

No comments:

Post a Comment