Tuesday, December 8, 2009

TANGANYIKA NAYO YAINGIA NUSU FAINALI CHALENJI

Timu ta taifa ya Tanganyika Kilimanjaro Stars imefanikiwa kuungana na ndugu zao wa Zanzibar ,Zanzibar Heroes kwa kuingia katika nusu fainali ya mashindano ya chalenji yanayoendelea kuunguruma huko Nchini kenya.


Alikua ni John Boko alipowainua washabiki wa Kili Stars katika dakika ya 62 alipoipatia timu hio bao la kwanza kabla ya Mshambuliaji machachari wa Kili Stars Mrisho Ngasa kuweka nyavuni goli la pili katika dakika ya 65, ikiwa ni tofauti ya dakika 3 tu tangu goli la mwanzo kuingia.


Mrisho Ngasa kwa mara nyengine tena akawainua washakiti wa Kili Stars alipoweka kimyani goli la tatu mnamo dakika ya 78, huku akionekana kuwa na uchu sana wa magoli pale alipoididimiza Eritrea kwa kufunga bao la nne kwenye dakika ya 85 na hivyo kufanya idadi ya magoli kwa Kili kuwa 4 - 0 kwa Eritrea

No comments:

Post a Comment