Wednesday, December 9, 2009

NI UPI UKWELI WA TAREHE 9 DISEMBA, UHURU WA TANZANIA AU TANGANYIKA?

Miaka 48 ya Uhuru wa Tanzania

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi, Jakaya Mrisho Kikwete, leo ameongoza maelfu ya Watanzania kuadhimisha miaka 48 ya Uhuru wa Tanzania, sherehe hizo zilifanyika leo katika Uwanja wa Uhuru a.k.a Shamba la.................


CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

MIAKA 48 YA UHURU: Kikwete kukagua gwaride maalum

Na Richard Makore

9th December 2009

Rais Jakaya Kikwete, leo anatarajia kukagua gwaride maalum la vikosi vya ulinzi na usalama katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru.

Tanzania leo inatimiza miaka 48 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Waingereza Desemba 9, mwaka 1961.

CHANZO: NIPASHE


Hivi ni baadhi ya vipande vya habari zilizochapishwa na magazeti ya Tanganyika leo asubuhi.

Kama tunavyojua leo ni ni tarehe 9 Disemba ndugu zetu wa Tanganyika wanaadhimisha miaka 48 ya uhuru wa nchi yao, laini jambo lakushagaza ni kwamba vyombo vingi vya habari vimekwepa kuchapisha ukweli halisi kwamba, leo ni siku ya uhuru wa Tanganyika na badala yake wakachapisha habari kuwa leo ni Uhuru wa Tanzania.

Mimi binafsi yangu nina maswali mengi ambayo najiuliza bila ya kupata jibu, kwa sababu kama mtakubaliana na mimi, basi mimi kwa jitihada yangu ya kusoma historia sijawahi kuona kama Tanzania iliwahi kutawaliwa, sasa unaposikia kwamba Tanzania inasherehekea miaka 48 ya uhuru, kwanza inafaa ujiulize Tanzania ilitawaliwa lini? na ni nani aliewahi kuitawala hio Tanzania hadi kufikia kuipa uhuru wake?

Jambo jengine mimi linalonipa utaa ni kwamba tangu hili neno Tanzania limeundwa kwa kuzishirikisha nchi mbili Tanganyika na Zanzibar basi halijatimia miaka 48 vyereje leo watu watangaze kwamba Tanzania imetimia miaka 48?

Pia kama nitakua sio mkosa najua kua hio Tanzania ni muungano wa nchi mbili, na kilamoja kati ya hizi nchi, iliwahi kutawalia na kupata uhuru wake kwa siku tarehe na miaka tofauti.

Tanganyika 9 Disemba 1961 na Zanzibar 10 Disemba 1963, na baada ya kila moja kupata uhuru ndipo nchi mbili hizi zikachukua hatua ya kuungana hapo mwaka 1964 na mwaka huo huo likaundwa neno Tanzania, na hapa hatuna haja ya kuujadili huo muungano wenyewe, sasa watu wenye elimu zao wanaposema kwamba uhuru wa Tanzania ina maana wamevifananisha visiwa vya Zanziba ni sawa sawa na vile vya mafya?. kwa sababu mimi naamini kwamba hawakuandika maneno haya kwa kusea

Na kama ni hivi mimi nahisi hapa kuna njama maalum za kutimiza ile azma ya watanganyika wanaoota ndoto ya kuifuta Zanzibar katika ramani ya dunia.kwa sababu walianza kwa vitendo vya chini kwa chini na baadae wakatangaza kwa maneno na sasa hivi wameamua kuutangazia ulimwengu kwa maandishi ya kua Tanzania hakuna kitu kinachoitwa Zanzibar, hili hutaliona kama ukiangalia juu juu inataka uangalizi wa macho ya ndani sana.kwa sababu hizi habari sio kama zinaishia tu ndani ya Tanzania, ispokua dunia nzima wanasoma hizi habari.

Ningependa kuwahadharisha wazanzibari wenzangu kuwa makini juu ya suala hili na hasa kwa wale watakaopata nafasi ya kuwachagua viongozi watakaoiongoza nchi yetu kwaa miaka ijayo, kama tusipokua waangalifu hili lengo lao la kuifuta Zanzbira linaweza kufanikiwa kwa asilimia 100, kwa sababu hivi sasa limeshatimia kwa asilimia fulani bila ya sisi wenyewe kujijua, na hii ni kutokana na viongozi wetu waliopo madarakani kufumba midomo yao kila mara inapotokea kitendo cha kuidhalilisha Zanzibar kwa njia moja au nyengine.

Mungu ibariki Zanziba na watu wake.

No comments:

Post a Comment