Tuesday, December 8, 2009

112 WAUWAWA NA WENGINNE 200 WAJERUHIWA BAGHDAD

Gari mbili zilizotegeshwa mambomu zimeripuka mjini Baghdad, moja iliripuka karibu na ofisi za wizara ya mambo ya ndani ya Iraq na moja iliripuka karibu na checkpoint ya polisi kusini mwa mji wa Baghdad.

Miripuko hio mikubwa imesababisha vifo vya watu 112 hadi sasa na wengine 200 wakijeruhiwa vibaya,mripuko wa mwanzo ulitokea mnamo majira ya saa 10:25 am. sawa na 08:25 CET wakati mripuko wa pili ulitokea dakika chache baadae.

Wanafunzi 6 wamepoteza maisha katika miripuko hio baada ya mripuko mmoja kutokea katika skuli na polisi 3 pia wameripotiwa kuuwawa katika miripuko hio.

Televisheni moja nchini Iraq imeripoti kuwa kuna mripuko mmoja pia umetokea katika marikiti, lakini hadi sasa hakuna mtu yoyote anaetuhumiwa kwa miripuko hio.

Miripuko ya leo nchini Iraq imetokea baada ya bunge la nchi hio kupitisha sheria ya kufanya uchaguzi hapo machi 6 2010,

Mripuko mwengine uliripotiwa kutokea jana katika mji wa Baghdad uliosababisha wanafunzi 6 pia kupoteza maisha na wengine 41 kuumia vibaya, siku hio hio mtu mwenye bunduki pia aliripotiwa kuuwa watu 5 katika checkpoint iliopo karibu ya Tarmiyah kaskazini mwa mji wa Baghdad.


Majeshi ya kimarekani yapatayo 1150,000 yapo ndani ya Iraq lakini idadi hio inatajiwa kupungua na kufikia 50,000 ifikapo mwakani 2010 kabla ya kukamilisha mpango wa kuyaondoa majeshi yote ifikapo mwaka 2011

No comments:

Post a Comment