Messi amejiwekea rekodi ya kua mchezaji wa kwanza kutoka Argentina kushinda mpira wa dhahabu, Messi amejishindia mpira huo baada ya kupata alama 473,na kumshinda Christiano Ronaldo ambae alishika nafasi ya pili kwa kupata alama 233 Ronaldo ndie alieshinda mpira huo mwaka jana alipopata alama 240.
Mchezaji wa kiungo wa Bercalona Xavi nae alishika nafasi ya tatu kwa kujizolea alama 170, huku Andre Iniesta akiwa katika nafasi na nne kwa alama 149, na msambuliaji wa Internazionale Milan Samuel Eto'o akiwa nafasi ya tanokwa alama 75.
Wengine walioingia katika kumi bora ni pamoja na Kaka Real Madrid alam 58,Ibrahimovic Barcalona alama 50,Wyne Roone Kutoka Manchester United alama 35,Didier Drogba alama Chelsea alama 33,pamoja na kiungo mkali wa Liverpool Steven Gerrard alama 32.
Messi alisema kua anajivunia ushindi huo kwa kua ni mtu wa kwanza kutoka Argentina, na vile vile atapata nafasi ya kuwekwa katika orodha ya wachezaji wakubwa duniani kama vile Zenedine Zidane, Johan Cruyff,Franz Berckenbauer,pamoja na Michael Platini.
"Ingawa kwamba walioshinda mprira huu ni wachezaj wakubwa lakini pia kuna wachezaji wakubwa hawakuwahi kushinda"alisema Messi.
Mchezaji wa mwanzo kushinda mpira wa Dhahabu kutoka nje ya bara la ulaya alikua ni Mliberia George Weah katika mwaka 1995 ambae alikua ndie mchezaji bora wa Dunia.
Kura zilizompa ushindi Messi hupigwa kila mwaka na waandishi wa habari za michezo kutoka nchi mbali mbali duniani, na anatarajiwa kukabidhiwa mpira wake katika Ghafla itakayofanyika siku ya jumapili nchini Ufaransa
No comments:
Post a Comment