Mahakama kuu Zanzibar imetoa uamuzi wa kupigwa mnada kwa hoteli inayomiliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayojuilikana kwa jina la Holeli ya Bwawani,uamuzi huo ulitolewa na Mrajis wa mahakama kuu ya Zanzibar Yesaya Kanyange kufuatia Serikali kushindwa kulipa deni la shilingi Trilioni 1.6 za mchele waliopewa na kampuni ya Leamthore ya nchini Thailand.
Kesi hio kabla ya kuotlewa uamuzi ilichukua muda wa miaka miwili tangu mwaka 2007 pale kampuni hio ilipofungua kesi mahakamani dhidi ya serikali kwa kushindwa kulipa deni la dola za kimarekani $60.4m na kutaka walipwe riba ya asilimia 25 pamoja na gharama zote za kesi,imesemwa kua kiasi hicho cha fedha kinachodaiwa dhidi ya Serikali ni sawa na bajeti ya miaka mitatu ya Serikali ya Mapinduzi.
Mrajis huyo wa mahakama kuu ameshaiandikia barua kampuni ya mnada ya kumekucha tayari kwa kuanza zoezi hilo, awali katika hukumu yake mahakama iliamuru kupigwa mnada kwa shamba la Serikali liliopo maeneyo ya kijichi lakini zoezi hilo lilishindikana kwa kutofahamika vizuri kwa mipaka ya shamba hilo.
Hukumu hio ilitolewa baada ya liyekua Katibu mkuu wa wizara ya fedha kwa wakati huo Bwana Omar Sheha kutohudhuria mahakamani,hata hivo Serikali ingelifanikiwa kuinusuru hoteli hio kwa kukata rufaa lakini wakati inajikurupusha kufanya hivo muda ulikuwa umekwisha.
Serikali iliingia mkataba na kampuni hio kipindi cha uongozi wa marehemu Idrisa Abdull Wakil na waziri kiongozi akiwa ni Seif Sharif Hamad.
Tayari kumekua na fununu kuwa baadhi ya wafanya biashara wakubwa wa Zanzibar wameonesha nia ya kutaka kuinunua hoteli hio iliyojengwa mara tu baada ya mapinduzi mwaka 1964 chini ya wa uongozi wa rais wa awamu ya kwanza ya Mh. Abeid Amani Karume
No comments:
Post a Comment