Monday, November 30, 2009

KIATU AME BINGWA MBIO ZA PUNDA ZANZIBAR

Wiki iliyopita wakaazi wa wa Mkoa wa mjini magharibi hasa wale wa wilaya ya mjini walishuhudia burudani mwanana ya mbio za punda iliyofanyika katika mji huo.Mbio hizo zilizoanzia viwanja vya kibanda maiti na kumalizikia katika uwanja wa Mao tse tung, ziliwashirikisha punda 60.

Mbio hizo zilizoandaliwa na kituo cha radio cha Coconut FM zilikua ni kivutio kwa watu waliofika na kushuhudia uhondo huo,kwani ni miaka miwili sasa mashindano hayo hayajaonekana tangu yalipofanyika kwa mara ya mwisho mwaka2007.

Mshindi wa kwanza wa mbio hizo aliejuilikana kwa jina la Kiatu Ame amejinyakulia zawadi mwanana ya shilini milioni moja (1,000,000) baada ya kutumia dakika 35:06 kwa kilomita sita,huku nafasi ya pili ikishikiliwa na kijana Makame Khamis aliyetumia dakika 36:00 na kunyakua shilingi laki saba (700,000).

Nafasi ya tatu ya mashindano hayo ilichukuliwa na Mwinyi Said na kuzawadiwa shilingi laki tano (500,000) wakati Abdullah Khamis alijipongeza kwa kitita cha shilingi laki mbili (200,000) kwa kutokea wa nne

Mgeni wa heshima katika mashindano hayo alikua ni Mstahiki mea wa mji wa Zanzibar Mahboub Juma.

2 comments:

  1. Hizi mbio za punda ziendelee...safi sana, zitawapunguzia wale vijana pale mbele ya skuli ya lumumba kuvuta bangi na kuwa mateja...

    ReplyDelete
  2. hahahahahaaaaaaaaaaaaaa au ndo wakipata hizo pesa watazidisha?

    ReplyDelete