Wednesday, December 2, 2009

MAJINA 10 YATAJWA KUWANIA TUNZO YA MWANAMICHEZO BORA EUROSPORT YAHOO 2009

Majina ya wanamichezo 10 kutoka katika fani mbali mbali duniani yametajwa tayari kwa kuwania tunzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2009 inayoandaliwa na utangazaji la Eurospot Yahoo, majina hayo yatahitaji kupigiwa kura kupitia katika mtandao wake wa Euro sport na matekeo yake kutangwaza siku ya tarehe 31 Disemba, wanamichezo hao ni kama wanavyoonekana kwenye picha pamoja na majina na fani zao.
Valentino Rossi ni muendesha pikipiki (moto GP) kutoka Italy na ameshashinda mashindano ya dunia mara saba.
Usain Bolt ni mwana riadha kutoka Jamaica ndie bingwa wa dunia na pia anashikilia rekodi ya kwenda kwa kasi zaidi kwa sasa kwa mbio za mita 100 ambapo alikimbia kwa dakika 9:19 pamoja na mita 200 ambapo alikimbia kwa dakika 19:19 pia ni bingwa wa mbio hizo kwa mashindano ya Olympic ambazo nazo pia amevunja rekodi kwa kwenda kwa kasi zaidi
Kim Clijsters ni mcheza tenis ambae alitangaza kujiuzulu miaka miwili iliopita lakini na sasa amerudi tena mchezoni
Andrew Strauss ni mcheza Criket kutoka England ambae pia ni nahodha wa timu ya taifa ya England kwa mchezo huo
Manny Pucquiano mpiganaji box kutoka philipines, ni bingwa wa dunia wa boxing katika uzito wa lightweight
Lindsey Vonn ni mmarekani anaecheza mchezo wa kuteleza katika milima ya mabarafu (alpine skiing) ambae anashikilia taji la dunia la mchezo huo kwa wanawake, alishawahi mara mbili kushiriki katika mashindano ya Olympic lakini hajawahi kushinda mara zote hizo kutokana na kuumia.
Jenson Button ni dereva kutoka England ambae anashiriki mashindano ya Formula 1,Jenson hakutajiwa kama angeendesha gari katika mashindano ya dunia 2009 lakini hatimae ndie alieibuka mshindi.
Casta Semenya mwanariadha wa kike kutoka Afrika kusini mwenye umri wa miaka 18 ambae alitikisha vyombo vya habari kutokana na jinsia yake kua na utata baada ya kushinda katika mashindano ya dunia yaliofanyika Ujerumani, na hatimae shirikisho la riadha duniani kupelekea kumchunguaza jinsia yake.
Alberto Contador muendesha baikeli kutoka Spain ambae alichukua ubingwa wa Tour de Frans mwaka jana akiwa na timu yake ya Astana, lakini akashinda kutetea ubingwa wake katika mashindano hayo mwaka huu 2009
Ryan Giggs ni mwanasoka kutoka Weles ambae alijiunga na Manchester United mwaka 1992, hadi sasa ameshacheza mechi 800 akiwa na mashetani hao wekundu na kati ya hizo ameanza katika kipindi cha kwanza mechi 700, hadi sasa ameshatikisha nyavu mara 150, pia keshapata zawadi za ubingwa wa England mara 11.
Kama unataka kumpigia kura mwanamichezo yoyote kati ya hawa basi ingia katika link ifuatayo ikisha nenda chini kwenye sehemu kipengele cha VOTE:

No comments:

Post a Comment