Thursday, December 3, 2009

MAURESMO ATANGAZA KUACHA TENIS

Aliekua bingwa wa dunia wa mchezo wa tenis mwaka 2004 Amelie Mauresmo ametangaza kujiuzulu mchezo huo.
Mauresmo ambae anajiuzulu mchezo wa tenis akiwa na umri wa miaka 30, kwa sasa anashikilia nafasi ya 21 duniani, ameshawahi kushinda kombe la Wimbledon pamoja na Australia open mwaka 2006, pia alishinda mashindano ya ndani ya Paris open mwezi Febuari mwaka huu.
"Nimekuja hapa kutangaza kujiuzulu,na nimefanya uamuzi huu baada ya kufikiria kwa makini" Mauresmo alisema maneno hayo na baadae akaanza kutokwa na machozi.

Hajashiriki mashindano mawili kwa mwaka huu tangu mwezi Septemba alipoumia katika mashindano ya US open alipokua akicheza na Aleksandra Wozniak.

Mauresmo alianza kucheza tenis ya kulipwa mwaka 1993 na ameshawahi kuchukua ubingwa wa WTA kwa mara 25

No comments:

Post a Comment