Monday, December 14, 2009

BERLUSCONI AVUNJWA MENO MILAN

Waziri mkuu wa Italy bwana Silvio Berlusconi amefikishwa hospitali moja mjini Milan baada ya kushambuliwa usoni na kusababisha uso wake kujaa damu

Waziri mkuu huyo mwenye umri miaka 73 amepata athari za kuvunjika meno pamoja na kupasuka sehemu za pua na mdomo baada ya mtu mmoja aliyekua karibu yake kumrushia chuma cha uso, baada ya shambulio hilo Berlusconi alitaka kuwahahakikishia wafuasi wake kwamba hakua na matatizo makubwa.

Massimo Tarlaglia mwenye umri wa miaka 42 ambae amefanya shambulio hilo ameshitakiwa kwa kosa la kumshambulia kiongozi wa nchi, uchunguzi unaonesha kuwa Tarlaglia ana matatizo ya akili, polisi walisema bwana huyo hakua na kumbu kumbu za uhalifu.

No comments:

Post a Comment