Sunday, November 15, 2009

KWANI WAO WAMEWEZA WANA NINI HATA SISI TUSHINDWE TUMEKOSA NINI?

Ni miongoni mwa barabara za wenzetu zikiwa katika mpango ulio bora kabisa, na ukizingatia kwamba wao hawana dhahabu, hawana almasi, hawana tanzanite, hawana shaba wala chuma.Hawana gesi hawana karafuu hawana mafuta ya petroli wala ya taa, wala hawazalishi kitu chochote chenye thamani duniani. Inauma sana

2 comments:

  1. Suali pengine ujiulize hao viongozi kila siku wako ziarani hawajaona jinsi barabara zinavojengwa?Ofcourse wanaziona, lakini wakienda nyumbani hujenga moja tuu...mwenda kwa miguu, baiskeli,gari kila kitu!

    Aidha wenzetu wamejaaliwa akili pengine sio mali nyingi, lakini wamepewa akili.Walikuja Afrika wakaiba mali zote za Afrika wakati wa ukoloni na kujenga makwao...wakati waafrika tukiwa tumelala!

    kwa hiyo shk Ommykiss wala usishangae kuwa hawana kitu, sie tumepewa mali lakini hatukupewa akili.

    ReplyDelete
  2. hapa kweli naungana na wewe kusema kwamba sisi wenye mali hatuna akili kwa sababu karume alikaa madarakani kwa muda usiozidi miaka minane kama sijakosea lakini alijenga majumba ya michenzani Unguja na Pemba mjini na mashamba na tangu afariki dunia tumeshapata marais watano baada yake na wamefanya (finishing ) ya majumba mawili tu ya michenzani kwa takriban miaka isiopungua 37 ni aibu ilioje.

    ReplyDelete