Sunday, November 15, 2009

MAFUNZO YACHUKUA NAFASI YA AZAM TUSKERShirikisho la soka nchini TFF limeichagua klabu ya Mafunzo kutoka kisiwani Zanzibar kuziba nafasi iliyoachwa na Azam kwenye michuano ya Tusker itakayoanza kutimua vumbi DesemGazeti moja la kila siku limeandika kuwa, hatua hiyo imekuja baada ya ZFA kuliandikia barua shirikisho hilo kuwa ingekuwa sawa kama nafasi hiyo ya nne ingechaguliwa timu moja kutoka kisiwani humo.

Mkurugenzi kamati ya ufundi, Sunday Kayuni amesema baada ya kugundua kuwa waliteleza kwa kuiteua Azam ndiyo maana nafasi hiyo wakaipeleka Zanzibar.

''Mashindano haya ni makubaliano kati ya wadhamini na TFF kwa hiyo katika uteuzi wa awali iliangaliwa ligi hii inayoendelea sasa na kuchaguliwa timu hizo nne, alisema Kayuni.

Alisema katika mashindano ya mwaka huu Uganda haitakuwa na timu shiriki wakati timu mbili zitatoka nchini Kenya ambazo ni Tusker pamoja na Sofapaka.

Timu zitakazoshiriki michuano hiyo ni pamoja na Yanga, Simba, Mafunzo pamoja na Mtibwa ambao ndiyo bingwa mtetezi.
ba 14 hadi 27.

No comments:

Post a Comment