Sunday, November 8, 2009

KISA CHA DA'I NA BABA YAKE IMAM

Ndugu zangu wapendwa,
Assalaam Alaikum Wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Bila shaka ukisoma kisa hiki utalowa kwa machozi kama vile hisia hizo zilivonipata. Naomba Mwenyezi Mungu Atuongoze katika njia nyoofu na Atuzidishie Imani katika dini yetu hii na kwa jitihada kubwa tumuamini Yeye Allah SWT. Amiin ya Rabbil ‘Alamiin
Kwa yeyote ataesoma, basi aitangaze kwa namna yeyote ili wengine wafaidike.

Fanyeni subra na someni hadi mwisho.

Qur’an 3:104: Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa

Qur’an 16:125 Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka

Kisa cha Da’i na Baba yake Imam
Kila Ijumaa adhuhuri baada ya salaa na Huduma za Ijumaa katika Msikiti Mkuu, na punde baada ya kipindi cha mafundisho ya “familia” (al Usrah), Imamu na mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka kumi na moja, hutoka na kwenda nje mitaani kugawa vitabu vidogo vidogo kuhusu “NJIA YA PEPONI” na vitabu vingine vya mafundisho ya Kiislamu.
Katika adhuhuri yenye kheiri ya Ijumaa moja, wakati ulipofikia Imam na mwanae kwenda kugawa vitabu, hali ya hewa nje ilibadilika na kuwa baridi kali na mvua kubwa.
Mtoto yule alijitayarisha kwa mavazi yake ya kumhifadhi joto na mvua, kasha akasema, “OK baba, mimi ni tayari”
Imam, Baba yake akauliza, “uko tayari kwa ajili gani?” “Baba ni wakati kukusanaya vitu vyetu na kwenda nje” Baba yake akasema, “Mwanangu, nje kuna baridi kali na mvua kubwa” Mtoto yule akamtizama baba yake kwa mshangao. Na akasema, “ baba, watu hawatoingia Motoni kama mvua ina nyesha?”
Baba akajibu, “mwanagu sitoweza kutoka nje na hali ya hewa kama hii!”
Kwa kusononeka, mtoto akamuomba baba yake, “ baba mimi naweza kwenda mwneyewe?” Baba yake alisita kwa muda kisha akasema, “mwanangu unaweza kwena, vitabu hivi hapa. Uwe muangalifu” “Shukran baba.”
Baada ya hapo mtoto yule alitoka nje katika mvua ile. Mtoto huyo wa miaka kumi na moja alipita mitaa ya mji ule akigonga mlango hadi mlango akigawa kitabu kwa kila alie kutana nae.
Baada ya masaa mawili hivi kutemebea katika mvua, alilowa chepe na kupata baridi kali, aligawa hadi nakala ya mwisho aliyo bakia nayo mkononi. Alisimama katika pembe moja na akitizama kama kuna mtu atatokea ili aigawe nakala ile iliyobakia, lakini mitaa ilikuwa kimya kabisa bila wala mtu mmoja.
Aligeuka kuelekea katika nyumba ya mwanzo aliyo iona karibu na kuanza kutembea pembezoni kuelekea katika mlango wa mbele, ailgonga kengere, lakini hakuna alieitikia. Aligonga tena na tena laikini hakuna aliejibu. Alisubiri lakini bila jibu. Mwishowe. Mtoto huyo (Daa’i), aligeuka kutaka kuondoka lakini akahisi kitu na kusubiri. Tena aliugeukia mlango na kugonga kengere na kugonga malango kwa mkono wake kwa sauti kubwa. Alisubiri kidogo, kuna kitu alichohisi kutoka katika ukumbi wa mbele wa nyumba ile. Aligonga tena, mara hii mlango ulifunguliwa taratibu.
Aliesimama mlangoni ni mwanamke mtu mzima alie onekana ni mwenye masikitiko. Aliuliza kwa ulaini, “Nikusaidie nini mwanangu?” Kwa uso mkunjufu na tabasamu, mtoto yule akasema, “Mama samahani kama nimekusumbua, lakini napenda kukuambia kwamba Allah kwa hakika Anakupenda na Anakulinda, na nimekuja tu kukupa kitabu changu cha mwisho ambacho kitakufundisha yote kuhusu Allah na nini lengo la Uumbaji na vipi upate Faraja Zake” Mtoto yule alimpa mama yule kitabu na kugeuka kuanza kuondoka.
Mama yule alimwita (mtoto) wakati anaondoka, “Ahsante mwanangu! Na Mwenyezi Mungu Akubarikie”
Ijumaa iliyofuatia baada ya Salaa ya Ijumaa, katika kipindi kile cha wiki cha “familia”, Imamu alitoa Da’wa kama kawaida yake. Alipomaliza aliuliza, “kuna mtu ana swali lolote au ana kitu che chote anataka kusema?”
Taratibu, kutoka safu ya nyuma ya wanawake, sauti ya mtu mzima ilisikika katika spika. Sauti nzuri , safi na furaha ilio kuwa dhahiri japokuwa haonekani, alisema, “Hakuna katika mkusanyiko huu anae nifahamu wala sijawahi kuonekana humu, hapo qabla. Ijumaa iliyopita sikuwa Muislamu na nilifikiri ningekuwa. Mume wangu alifariki muda umepita. Aliniacha peke yangu katika dunia hii. Ijumaa iliyopita, vile ilivyokuwa siku ya baridi na mvua, basi ilikuwa kushinda hivyo ndani ya moyo wangu, kiasi kwamba nilifikia kikomo cha matumaini ya kuishi.
Hivyo nilichukua kamba na kiti kupanda ngazi hadi kufikia sakafu ya juu ya nyumba yangu. Niliifunga kamba imara katika mwamba wa wa sakafu lile la juu, kisha nikasimama juu ya kiti na kuifunga upande wa pili wa kamba katika shingo yangu. Nilisimama juu ya kiti kwa upweke na niliye vunjika moyo. Nilikuwa karibu kutegua kiti, pale kwa ghafla nilisikia mlio mkubwa wa kengere ya mlangoni kutoka chini ikinikera. Nikafikiri kuwa yeyote ataekuwa atakwenda zake. Nilisubiri na kusubiri lakini sauti ya kengere ilizidi na kukazana, kisha mtu anaegonga kengere alianza kugonga mlango kwa sauti kubwa. Nikajisemea, ‘nani katika dunia hii anaweza kuwa? Hakuna mtu alisha wahi kugonga kengere wala kuja kunitizama’ Niliiregeza kamba shingoni, nikaivua na kushuka chini hadi mlango wa mbele. Wakati wote huo sauti ya kengere ilizidi.
Nilpofungua mlango na kutizama, sikuamini macho yangu kumuona mvulana mzuri mwenye furaha amabe sijawahi kumuona katika maisha yangu. Tabasamu yake. Oh! siwezi kuifafanua. Maneno aliyo nitamkia yaliufanya moyo wangu ulio kuwa umekufa muda mrefu, KUIBUKA KATIKA UHAI, kwa sauti yake ya ajabu, “Mama nataka tu kukuambia kwamba ALLAH KWA HAKIKA ANAKUPENDA NA ANAKULINDA” Kisha alinipa hiki kitabu, “Njiia ya kwenda Peponi” ambacho hivi sasa ninacho mkononi.
Mtoto yule (Malaika) mwema alivotoweka ndani ya baridi na mvua ile, nilifunga mlango na nikasoma kwa uangalifu kila neno ndani ya kitabu hiki. Kisha Nilirudi juu kuchukua kamba yangu na kiti changu. Sikuvihitajia tena.
Mnafahamu? Sasa mimi ni mwenye furaha na mwenye kumuamini Mungu Mmoja. Kwa kuwa anwani ya mkusanyiko huu imeandikwa nyuma ya kitabu hiki, nimekuja hapa mwenyewe kukushukuru kwa Mwenyezi Mungu wa Malaika yule mdogo ambae alikuja katika sekunde za muda wa mwisho na kwa kufanya hivo alisalimisha roho yangu isiingie katika Moto wa milele.
HAKUKUWEPO MACHO MAKAVU TENA HUMO MSIKITINI. Saut za TAKBIIR, ALLAHU AKBAR, zilipaza hewani hata miongoni mwa wanawake pia.
Imam, Baba alishuka kutoka katika mimbari hadi katika safu ya mbele sehemu aliyo kuwa ameketi malaika yule mdogo. Alimchukua mwanae na kulia bila kujizuia.
Bila shaka hakuna jamaa iliyowahi kupata kipindi chenye furaha kama hiki, na bila shaka ulimwengu haujawahi kamwe kuona Baba ambae alijaa na mapenzi na radhi ya mwanae, ila mmoja, huyu mmoja.

Macho yenu yabarikiwe kwa kusoma kisa hiki. Msikifanye kisa hiki kikapotea, someni tena na tean na muwanufaishe wengine. Pepo ni kwa ajili ya Watu wake.
Kumbuka kwamba, Resala ya Mwenyezi Mungu hufanya mabadiliko katika maisha ya mtu alie karibu nawe. Isambaze resala hii kwa wingi uwezavyo.
Sambaza Resala za Mwenyezi Mungu na utaona manufaa kwa kila ufanyacho.

Qur’an:5:3 ……..Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu

Qur’an:3:110 Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu

Aya zingine katika Qur’an: 29:46; 4:82; 60:8; 3:111; 39:19

Bibilia
Is 43:11; Ez 1820; Joh 5:30; Act 2:22; Joh 17:3; Jam 2:17; finally, Jer 8:8.

Mwenyezi Mungu Akujaaliyeni muwe wenye kufuzu hapa duniani na huko Akhera, Amiin

No comments:

Post a Comment