Saturday, November 14, 2009

KIFICHO AWAOMBA MAHUJAJI KUSAMEHEANA


Spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar Alhaj Pandu Ameir Kificho amewataka wananchi wanaojiandaa kwenda kutekeleza ibada ya hija kusameheana kabla ya kwenda kutekeleza ibada hio katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
Alhaj Kificho aliyasemma hayo jana alipokua akizungumza katika semina ya maandalizi ya mahujaji wa mwaka huu 2009 ilioandaliwa na Al-Haramain Hajj Group, wakishirikiana na Jumuia ya Maimam Zanzibar,katika hotuba yake hio kificho alisema kusameheana ndiko kunakojenga umoja nidham na mshikamano.
"Sisi kama binaadam tunafanya makosa, makosa ambayo yanapelekea kutoelewana baina yetu katika jamii, na ni kosa kwa mtu kula kiapo cha kutokusamehe.
Mahujaji wapatao 153 wanatarajiwa kuhudhuria katika semina kwa ajili ya matayarisho ya hija, ambazo zitaishia manamo mwisho wa mwezi huu wa Novemba.Hija ni nguzo moja kati ya nguzo tano za kiislam, ambayo kila muislamu mwenye uwezo anapaswa aitekeleze angalau mara moja katika uhai wake.
Kila mwaka waislamu wapatao milioni mbili wanahudhuria ibada ya hija huko Makka sehemu tukufu kuliko zote katika Uislam.

No comments:

Post a Comment