Saturday, November 14, 2009

ELIZABETH ASEMA WATANZANIA WAMEMUANGUSHAMSHIRIKI wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta amewalawahumu Watanzania kwa kushindwa kumpigia kura za kumbakiza ndani ya jumba hilo ambalo mshindi atajinyakulia kitita cha dola 200,000.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Elizabeth alisema kuwa nchi tano zilimpigia kura, lakini Tanzania ilimuangusha kwa vile mashindano hayo wanaangalia zaidi kura zinazopigwa nchini mwako.

“Uganda, Kenya walinipigia, lakini Tanzania kura zilikuwa chache, halafu mashindano ya mwaka huu ni magumu tofauti na miaka mitatu iliyopita, safari hii washiriki ni 25 sheria zimebadilika,” alisema. Elizabeth aliongeza hakuwa na uhusiano na mshiriki mwenzake Kelvin wa Nigeria na kudai kuwa urafiki wao utabaki kuwa wa kawaida na si vinginevyo.

Eliza alisema “Kuishi na watu kazi sana kila mtu ana tabia zake, ukizingatia hakuna mawasiliano mimi sikuwa naigiza ndio tabia yangu ilivyo, lakini wapo ambao wanaigiza ingawa wote lengo letu ni kusaka fedha.

Akizungumzia minong’ono inayodaiwa kuwa yeye ni mjamzito au kabakwa alisema “ni kitu kinachoniuzunisha sana uwa kinaniliza kwa kuwa sikupata muda wa kusikilizwa, ingawa mimi nilisikiliza:

“Kubakwa si siri ila ni kitu kibaya kinahuzunisha, na mimba pia si siri kwani huwezi kuificha kwa sababu itakuja kuonekana, nilitaka niiseme siri inayoniumiza nikiwa BBA nikijua watazamaji watanisikia, lakini sikuweza kusema, kwa sasa bado iache iwe siri ipo siku nikijisikia kusema nitaisema.

Na aliweka wazi kauli yake ya kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na mtu ambaye sio halfcast na akadai sio chuki ilopelekea yeye kusema hivyo bali ile ni reality show na alikuwa anaeleza historia ya maisha yake na huo ndo ukweli kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na na mwafrika

No comments:

Post a Comment