Wednesday, November 11, 2009

JE HII NDIO KAZI YA JESHI LA KUJENGA UCHUMI (JKU)?


Nijuavo mimi kazi ya hili jeshi la kujenga uchumi Zanzibar (JKU) kubwa ni kushughulikuia mashamba ya mipunga na mambo na mambo yanayofanana na hayo na sio kushughulikia mambo yanayohusu usalama wa raia, lakini katika picha hii askari wa JKU wanaonekana wakimpiga mikwaju raia huku wenye kazi ya usalama wa raia wakiwa pembeni, jee hapa JKU watakua na jibu gani juu ya hili kama si kufanya yasio wahusu

2 comments:

  1. hawa kazi yao kulima mpunga kule cheju na hanyegwa na sio kuonea raia bila sababu

    ReplyDelete
  2. Hapo kwenye picha nafikiri suala ni kwanini wanaendelea kumpiga mwananchi aliekwisha salimu amri?
    Kisheria wanatakiwa wamchukue na kumpeleka kwenye vyombo vinavyohusika kama ni mahakamani na kwengineko na sio kujichukulia sheria mikononi kwa kumpiga kama wanavyofanya kwenye picha hii.

    Wanachokifanya hapo ni kuvunja haki za binadaamu kwa kutesa wananchi wasio na hatia.Maana wanajua kama wakimpeleka mahakamani ataachiwa kwa vile hana kosa!

    ReplyDelete