Saturday, November 28, 2009

HII NDIO INAYOUA WATU CONGO

Dhahabu hii kutoka mashariki ya Congo eneo la Kaniola pamoja na maeneo mengine ndio yanayounda mlolongo wa matatizo ndani ya Congo. Biashara hii ya maadini ndio ilioleta vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha watu wengi kuikimbia nchi yao.Nchi ambayo ilitegemewa kuwa ni miongoni mwa nchi matajiri duniani.Inakisiwa kua Congo iliuza maadini mbali mbali ikiwemo Dhahabu kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni hamsini ($50m) mwaka jana.Katika biashara hii ya dhahabu ambayo wafanyakazi wake wakuu ni watoto,inawafaidisha wana wazungu pamoja na wakuu wa nchi huku ikiacha wananchi wake wakikosa huduma muhimu za kijamii.

No comments:

Post a Comment