Tuesday, September 29, 2009

MWAKILISHI WA CUF APANDISHWA KIZIMBANI

Mwakilishi wa chama cha wananchi ( CUF ) jimbo la chonga kisiwani pemba Mh Abdallah Juma Abdallah jana amepandishwa mahakamani katia mahakama ya mwanzo Wilaya ya Chake Chake kwa kosa la kumtolea maneno ya kashfa na matusi sheha wa shehia ya Pujini Bwana Khamis uledi kombo, katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chake Chake kufuatia utoaji wa vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi (Zan IDs). Mwendesha mashtaka Bwana Juma Habib aliiambia mahakama hio kwamba mwakilishi huyo alitenda kosa hilo siku ya tarehe 19 aug, mwaka huu na kutiwa hatiani kwa kifungu cha sheria  ya Zanzibar 74(1) (b) ya mwaka 2004 Hata hivyo mwakilishi huyo alikanusha kosa hilo na hakimu wa mahakama hio Ali Abdurrahman Ali alimwachia kwa dhamana ya sh,150,000 na kesi kuhairishwa hadi tarehe 15 oct 2009 itakaposikilizwa tena.

No comments:

Post a Comment